Advertisement
KANDANDA

Taifa Stars kucheza na Misri Jumapili kujiandaa na AFCON

Timu hiyo imepangwa Kundi D lenye timu za Morocco, Zambia na DRC katika fainali hizo za AFCON
Advertisement

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', itajipima ubavu Jumapili na Misri katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kujiandaa na michuano ya AFCON.

Advertisement

Mechi hiyo itakuwa ni ya kujiweka sawa kabla ya kuelekea nchini Ivory Coast kushiriki michuano hiyo ambayo inatarajiwa kuanza Januari 13.

Stars imepiga kambi nchini Misri ambapo imeweka kambi ya muda tangu mwanzo wa wiki hii wakiwa chini ya Kocha, Adel Amrouche.

Katika michuano ya Afcon, Stars itatupa karata yao ya kwanza kwa kucheza na Morocco, Januari 17 kisha itacheza na Zambia, Januari 21 na watamaliza mechi za makundi Januari 24 kwa kucheza na DRC.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro, ametangaza kamati maalumu ya hamasa ambayo lengo lake ni kuziwezesha timu za taifa.

Advertisement

Kamati hiyo imeundwa ikiwa inajumuisha majina ya watu mbalimbali wenye ushawashi katika jamii na baadhi ya viongozi wa mpira wakiwemo Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' ambao ni wajumbe.

Jukumu la kwanza la kamati hiyo itakuwa ni kuandaa hafla ya harambee ambayo inatarajia kufanyika Januari 10 jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atamuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama mgeni rasmi.

Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti, Theobald Sabi, Patrick Kahemele (Makamu), Neema Msitha (Katibu) na wajumbe ni Hersi, Try Again, Betrice Singano, Michael Nchimbi, Nicky Reynolds, Cristina Mosha ‘Seven’, Hamis Ally na Paul Makanza.

Wengine ni Mohamed Soloka, Mwijaku, Baba Levo, Jemedari Said, Lucas Mhavile ‘Joti’, Hassan Raza, Oscar Oscar na Prisca Kishamba.

Advertisement