Advertisement
Klabu Bingwa Afrika Wanawake

JKT Queens yapania kung'ara Klabu Bingwa Afrika

Timu hiyo itaanza kutupa karata yake ya kwanza kwa kuumana na Mamelodi Sundowns Ladies ya Afrika Kusini
Advertisement

Mabingwa wa soka la Wanawake Afrika Mashariki na Kati, timu ya JKT Queens, wanaondoka kesho kwenda Ivory Coast kwa ajili ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika inayotarajiwa kuanza Novemba 5.

Advertisement

Timu hiyo itaanza kutupa karata yake ya kwanza kwa kuumana na Mamelodi Sundowns Ladies ya Afrika Kusini.

Mamelodi ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo, ni miongoni mwa timu bora zinazoshiriki kwenye michuano ya mwaka huu na mchezo wao wa kwanza dhidi ya JKT Queens utapigwa siku hiyo kuanzia saa 5 usiku.

Akizungumzia na Pulsesports jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa JKT Queens, Masau Bwire, amesema maandalizi yote kwa upande wao kama uongozi yamekamilika na wanatarajia kwenda kushindana ili kufanya vizuri.

Amesema msafara wa timu yao unaondoka na baadhi ya wachezaji huku wachezaji wengine ambao wapo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Stars' ambacho kipo nchini Botswana wataungana na timu huko Ivory Coast.

Advertisement

"Sisi tumemaliza maandalizi yetu na tunasafiri tukiwa tunajiamini kwa kiasi kikubwa, kikosi kitaondoka kesho (leo) majira ya alfajiri na baadhi ya wachezaji waliopo kambini na wale ambao wapo kwenye timu ya taifa watajiunga na timu tukiwa huko Ivory Coast," amesema.

Mbali na mchezo huo dhidi ya Mamelodi Sundowns lakini JKT Queens watavaana na Athletico Abidjan ambao ni wenyeji kwenye mchezo wa pili ambao utapigwa Novemba 8.

Mchezo wa mwisho JKT Queens watamaliza na Sporting Casablanca ya Morocco mchezo ambao utapigwa Novemba 11.

Kama JKT watatinga hatua ya nusu fainali basi watashuka dimba Novemba 15 na tamati ya michuano hiyo inatarajiwa kuwa ni Novemba 18.

Advertisement