Simba yakiri mechi na Dynamos ngumu

© Kwa Hisani

KANDANDA Simba yakiri mechi na Dynamos ngumu

Zahoro Mlanzi • 19:21 - 27.09.2023

Simba SC ya Tanzania yajiandaa kwa mchezo mgumu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

KLABU ya Simba, imeweka wazi wapo tayari kwa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia lakini utakuwa mchezo mgumu kwao.

Mchezi huo utapigwa saa 10 jioni katika Uwanja wa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam huku kila timu ikijua katika mchezo wa kwanza zilifungana mabao 2-2.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally, amesema hawatakuwa na hamasa kubwa kuelekea mchezo huo kwakuwa uwanja huo kuwa na uwezo wa kubeba watazamaji 7,000.

“Kuelekea kwenye mchezo huo ambao ndio utafuatiliwa zaidi Afrika kwa wikiendi hii kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza. Ukubwa wa Simba SC ndio unafanya mchezo huo uwe mkubwa zaidi," amesema Ally na kuongeza.

“Kikosi leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex pale Chamazi kwa ajili ya kuzoea uwanja. Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wetu wengi wanaujua uwanja ule na wapo wengine hawaujui.

"Tunafahamu mchezo ni mgumu dhidi ya Power Dynamos, wote mliona namna walivyotusumbua lakini wanakuja nyumbani Tanzania, sehemu ambayo hakuna aliyetoka salama na hicho hicho atakutana nacho. Bora wangekubali tukamalizana nao kwao."

Ametaja viingilio katika mchezo huo kuwa ni mzunguko sh. 10,000, VIP B ni sh. 30,000 na Platinum ni sh. 150,000 ambayo utapata zawadi, usafiri, chakula ukiwa uwanjani.

Akizungumza ujio wa Dynamos, Ally amesema:"Power Dynamos wanatarajiwa kuwasili nchini kesho saa 12 jioni na Shirika la Ndege la ATCL. Waamuzi wanatarajia kufika Tanzania Septemba 30.

Ameongeza mechi hiyo wataitumia kama maandalizi ya kwenda kucheza CAF Football League.

Tags: