Advertisement
LIGI KUU

Baraza apewa mikoba kuinoa Dodoma Jiji

Kocha huyo alijijengea heshima kubwa katika soka la Tanzania baada ya kuiwezesha Biashara United kucheza michuano ya kimataifa
Advertisement

Timu ya Dodoma Jiji, imemtangaza kocha wa zamani wa Biashara United na Kagera Sugar, Francis Baraza raia wa Kenya, kuziba nafasi ya kocha aliyeondoka wiki iliyopita kikisoni hapo Melis Medo.

Advertisement

Kocha huyo ameingia kandarasi ya mwaka mmoja ya kukinoa kikosi cha timu hiyo ambayo iliachwa mikononi kwa Kocha Msaidizi, Kassim Liogope.

Kabla ya kujiunga na Dodoma Jiji, Baraza alikuwa akiinoa Polisi ya Kenya ambayo alitimuliwa Oktoba kutokana na kutokuwa na matokeo mazuri katika Ligi Kuu ya Kenya.

Dodoma Jiji ni miongoni mwa timu ambazo zilianza vizuri msimu wa Ligi Kuu Bara wakikusanya alama 15 katika mechi zao nane za awali lakini kwasasa wana mechi kadhaa hawajapata matokeo ya ushindi.

Kocha Baraza kesho kwa mara ya kwanza atapata fursa ya kukishuhudia kikosi cha timu yake kikipepeteana na Ihefu FC kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma lakini bado haijajulikana kama ataweza kusimama kwenye benchi la ufundi kwa ajili ya mchezo huo.

Advertisement

Baraza amewahi kutamba na kikosi cha Biashara msimu wa 2020-21 ambapo aliisadia timu hiyo kumaliza katika nafasi nne za juu na kwa mara ya kwanza wakapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

Hata hivyo baada ya mafanikio hayo, alipata fursa ya kuchukuliwa na timu ya Kagera Sugar ambayo alifanya nayo vizuri katika hatua zake za awali kabla ya mambo kubadilika na kutupiwa virago.

Anakichukuwa kikosi cha Dodoma Jiji ambacho kwasasa baada ya kushuka dimbani mara 12, kimekusanya alama 15 wakiwa nafasi ya 9 na mchezo wao wa mwisho wa ligi waliucheza Desemaba 3 katika Uwanja wa Majaliwa ambapo walikubali kichapo cha 1-0 kutoka kwa wenyeji Namungo FC.

Advertisement