Robertinho:Tutawatoa Al Ahly kwao

© Kwa Hisani

KANDANDA Robertinho:Tutawatoa Al Ahly kwao

Zahoro Mlanzi • 22:06 - 21.10.2023

Kocha huyo raia wa Brazil, amewasifu wachezaji wake kwa kuonesha mchezo mzuri licha ya kuwa walikuwa wanakabiliana na timu kubwa, bora na yenye uzoefu barani Afrika.

Kocha wa Klabu ya Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho', amesema bado timu yake ina nafasi ya kuwatoa Al Ahly kwenye mechi ya marudiano itakayopigwa Cairo, Jumanne ya wiki iyajo.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Pulsesports baada ya mechi yao dhidi ya Al Ahly iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2 katika michuano ya AFL Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Kocha huyo raia wa Brazil, amewasifu wachezaji wake kwa kuonesha mchezo mzuri licha ya kuwa walikuwa wanakabiliana na timu kubwa, bora na yenye uzoefu barani Afrika.

"Nimeridhika na kiwango cha wachezaji wangu wote, Al Ahly wametuzidi kwa vitu vingi ikiwemo uzoefu hivyo kuwapa mechi kama hii ni jambo la kujivunia kwangu na wachezaji," amesema.

"Kwasasa akili yetu tunaihamishia kwenye maandalizi kuelekea mechi ya marudiano na tunaweza kufanya vizuri zaidi kwani kwenye mpira hakuna kinachoshindikana," amemazilia Robertinho.

Katika mchezo huo, Simba walikuwa nyuma kwa bao 1-0 hadi mapumziko lakini walibadili matokeo na kusomeka 2-1 ndani ya dakika 10 baada ya kuanza kipindi cha pili.

Mabao ya Al Ahly yalifungwa na Reda Slim na Mahmoud Kahraba huku yale ya Simba yakifungwa na Kibu Denis na Sadio Kanoute.

Wakati huo huo, kikosi cha Simba, kinatarajia kuondoka nchini muda wowote kuanza sasa kwenda kukita kambi nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya marudiano ambayo itachezwa Oktoba 24.

Ushindi kwa Simba au sare ya mabao zaidi ya mawili ndio pekee utaweza kuwasaidia ili kufuzu kwenye hatua ya nusu fainali.

Tags: