Yanga kuzivaa Azam FC, Singida FG kwa Mkapa

© Kwa Hisani

KANDANDA Yanga kuzivaa Azam FC, Singida FG kwa Mkapa

Zahoro Mlanzi • 19:30 - 19.10.2023

Klabu ya Yanga imebadilisha ratiba ya mechi zao dhidi ya Azam na Singida FG, zitachezwa siku moja, mechi ya kwanza itakuwa Jumatatu.

Klbau ya Yanga, imethibitisha mabadiliko ya ratiba katika mechi zao mbili mfululizo za nyumbani za Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam na Singida FG ambapo sasa michezo hiyo yote imesogezwa mbele kwa siku moja.

Awali mechi ya Yanga dhidi ya Azam ilipangwa kuchezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam lakini sasa mchezo huo umesogezwa hadi Jumatatu sa 12 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi, mchezo wao dhidi ya Singida FG ambao ulipangwa kuchezwa Oktoba 26 kwenye Uwanja wa Azam, sasa utachezwa Oktoba 27 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 12 jioni.

Mabingwa hao watetezi ambao kwasasa wapo kambini kwao Avic wakiwa wanajifua vikali wanatarajiwa kuwa ni wenyeji katika michezo yote miwili.

Yanga kwasasa wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama zao 12 baada ya kufungwa mchezo mmoja kwenye mechi tano walizocheza hadi sasa.

Katika mechi yao ijayo wanakutana na Azam ambao hadi sasa hawajapoteza mchezo wowote kati ya mitano waliocheza na wapo kwenye nafasi ya pili nyuma ya Simba katika msimamo wakiwa na alama 13.

Wakati huohuo, Singida FG, imefurahia mchezo kuchezwakwa Mkapa na kwamba wataonesha ubora wao.

Akizungumza na Pulsesports, Ofisa Habari wa Singida FG, Hussein Massanza, amesema wao kama klabu wamefurahishwa kwani itakuwa muda mzuri kwa wachezaji wao kuonyesha ubora wao.

"Hii ni taarifa njema imekuja kwetu na tumefurahi sana, tutacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Mkapa, uwanja umefanyiwa maboresho makubwa, nyazi imekaa vizuri ni fursa ya kuonyesha uwezo wa akina Chukwu, Elvis Rupia, Tchakei," amesema Massanza.