Mashabiki 3 wafariki ajalini kuwahi mechi ya Namungo, Yanga

© Kwa Hisani

KANDANDA Mashabiki 3 wafariki ajalini kuwahi mechi ya Namungo, Yanga

Zahoro Mlanzi • 13:09 - 20.09.2023

Ajali hiyo imetokea eneo la Miteja karibu na Somanga na kusababisha vifo hivyo na majeruhi 30.

Klabu ya Namungo FC, imepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya mashabiki wao watatu waliofariki dunia wakiwa safarini kwenda Dar es Salaam wakitokea Lindi kushuhudia timu yao itakayoumana na Yanga SC leo saa 1 usiku.

Ajali hiyo imetokea eneo la Miteja karibu na Somanga na kusababisha vifo hivyo na majeruhi 30.

Namungo itakuwa ugenini kuumana na Yanga katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolew na klabu hiyo imeeleza:"Kwa sasa majeruhi wote wamepelekwa katika Kituo cha Afya Tingi Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi".

Klabu hiyo imetoa pole kwa wanaruangwa, mashabiki, familia na kwa wote waliopata ajali hiyo na majeruhi wanawaombea kwa Mungu wapone haraka.

Iliongeza Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahala pema peponi. Amina.