Taifa Stars ya kosa sh. bilioni 1.3 baada ya kubanduliwa AFCON

KANDANDA Taifa Stars ya kosa sh. bilioni 1.3 baada ya kubanduliwa AFCON

Zahoro Juma • 09:40 - 25.01.2024

Hiyo ilikuwa motisha katika kuhakikisha wachezaji wa Taifa Stars wanapambana katika kuandika historia mpya.

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', ilitoa sare tasa dhidi ya DR Congo na kukosa dola 500,000 za Kimarekani (zaidi ya sh. bilioni 1.5 za Kitanzania) iliyo ahidiwa na serikali endapo timu hiyo itafuzu 16 Bora ya AFCON.

Stars ilishika mkia Kundi F kwa alama 2, ilihitaji kushinda mchezo huo ili kufuzu hatua hiyo.

Kundi hilo liliongozwa na Morocco yenye alama 7 ikifuatiwa na DR Congo yenye alama 3 na Zambia iliyo na alama 2.

Kwa mujibu wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro, ahadi hiyo limetolewa Kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kuongeza hamasa kwa wachezaji.

Dkt. Ndumbaro aliaamini kupitia ahadi hiyo wachezaji watapambana hadi tone la mwisho ili kushinda na kuiweka Tanzania katika ramani mpya ya soka.

Mchezo huo ulipigwa Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Karhogo katika mchezo wa mwisho wa kundi F.

Mchezo mwingine wa kundi hilo ulikutanisha Morocco dhidi ya Zambia ambao ulichezwa kwenye Uwanja wa Laurent Pokou mjini San- Pedro.