Simba SC yamnasa beki wa Prisons

KANDANDA Simba SC yamnasa beki wa Prisons

Zahoro Juma • 21:00 - 17.01.2024

Usajili huo wa Simba, unafanya kufikisha wachezaji sita iliosajili katika dirisha dogo

Klabu ya Simba, imemtambulisha beki Edwin Balua, 22, kuwa mchezaji wao mpya wa sita dirisha hili dogo kutoka Tanzania Prisons ya Mbeya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa katika mtandao wa kijamii wa X wa klabu hiyo, Balua amesaini mkataba wa miaka mitatu.

Wachezaji wengine wapya ni viungo wawili, Msenegal Babacar Sarr, 26, kutoka US Monastir ya Tunisia na winga, Ladaki Chasambi, 19, kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Wapo pia washambuliaji, Muivory Coast, Freddy Kouablan, 25, kutoka Green Eagles ya Zambia ambako alikuwa anaongoza kufunga mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo.

Wengine ni Mgambia, Pa Omar Jobe, 25, kutoka Zhenis ya Kazakhstani na Saleh Karabaka, 23, kutoka JKU ya Zanzíbar.

Katika dirisha hili dogo Simba SC pia imeachana na washambuliaji wake wawili wa kigeni, Mkongo Jean Baleke na Mzambia na Moses Phiri, hivyo kufanya jumla ya wachezaji sita iliyowaondoa dirisha hili dogo.

Wengine ni wazawa viungo Jimson Mwanuke, 24, Nassor Kapama, 27, na washambuliaji Shaaban Chilunda, 25 na Mohamed Mussa, 22.

Tags: